Tatizo
la madawa ya kulevya limetokea kuwa janga kubwa duniani kote, watu
wengi wameathirika na janga hili. jinsia zote wanaume, wanawake, na
vilevile rika zote vijana na wazee pia.
Hapa tutaongelea aina mbili za madawa ya kulevya yaani Cocaine na Heroin.
Hapa tutaongelea aina mbili za madawa ya kulevya yaani Cocaine na Heroin.
Cocaine
Hutokana na majani ya mmea uitwao kitaalamuErythroxylum coca bush.
Hutokana na majani ya mmea uitwao kitaalamuErythroxylum coca bush.
Aina hii ya dawa ya kulevya hutolewa kwa mifumo ifuatayo;
Unga ambapo
mitaani hujulikana kama ‘coke’ na hutumika kwa kuvutwa puani kama unga,
au kuyeyushwa na maji na kuchomwa kwenye mshipa wa damu.Crack ambapo
mitaani hujulikana kwa jina hilohilo crack au rock, na hutengenezwa kwa
kuchanganywa na kemikali. Na hutumika kwa kuvutwa kama sigara.Cocaine
pindi inapoingia kwenye damu huenda kwenye ubongo na kuzuia ufyonzwaji
wa vihisishi vifuatavyo: dopamine, norepinephrine na serotonin, kutoka
kwenye ubongo. Hivyo ubakia kwenye ubongo. Na vihisishi hivi husababisha
ile hali ya furaha, mchangamfu na kujisikia mwenye nguvu kitaalamu
euphoria. Na huweza kuwa kwenye hali hii kwa nusu saa tu.
Mara tu baada kutumia dawa hii dalili zifuatazo hutokea
Mara tu baada kutumia dawa hii dalili zifuatazo hutokea
Mishipa ya damu
husinyaa (constricted blood vessels)Joto la mwili huongezekaMapigo ya
moyo huongezekaShinikizo la damuDilated pupils
Matumizi ya muda mrefu ya dawa hii ya kulevya huleta madhara yafuatayo; Pamoja na kwenda kwenye ubongo husambaa sehemu nyingine za mwili na mzunguko wa damu
Matumizi ya muda mrefu ya dawa hii ya kulevya huleta madhara yafuatayo; Pamoja na kwenda kwenye ubongo husambaa sehemu nyingine za mwili na mzunguko wa damu
1.Moyo - Kwenye
moyo huweza kuleta Shambulizi la moyo (heart attack) na vilevile mapigo
ya moyo yasiyo na mpangilio (Arrhythmia) hivyo unaweza kufa ghafla tu.
2.Ubongo -
Mishipa ya damu kwenye ubongo inaweza kusinyaa na kupelekea kupata
Kiharusi, hata kwa kijana. Vilevile unaweza kupata ugonjwa wa akili
(substance abuse pyschosis).
3.Mapafu na mfumo
wa hewa - Uvutaji kupitia pua huweza kupelekea tatizo sugu la kutokwa
damu puani kila wakati na mafua yasiyo pona, kupoteza mfumo wa harufu,
na ikivutwa kama sigara kuharibu mapafu moja kwa moja.
4.Mfumo wa chakula - Cocaine husababisha kusinyaa kwa
mishipa ya damu kwenye tumbo na utumbo hivyo kusababisha vidonda na
kuweza kuharibu kabisa mfumo huu kwa utumbo kuoza.
5.figo - kutokana na shinikizo la damu mafigo yanaweza
kushindwa kufanya kazi vizuri, vilevile cocaine inaweza kuleta madahara
moja kwa moja kwenye mafigo kitaalamu Rhabdomyolysis.
6.Ngono - ingawa cocaine huweza kutumika kama njia ya
kuongeza hamu ya ngono huweza kusababisha kushindwa kumaliza kile
ulichokianza. Matumizi sugu ya dawa hii ya kulevya huleta madhara kwa
jinsia zote yani kwa wanaume na wanawake.Na vilevile huweza kufanya kuwa
tegemezi wa dawa hii.Kwa wanaotumia sindano na kushea wanaweza kupata
maambukizi ya virusi ya hepatitis na vya ukimwi.
Nini hutokea baada ya matumizi ya muda mrefu ya kokeni?
Baada ya kutumia cocaine kwa muda mrefu punde unapoacha tu kutumia dalili zifuatazo hutokea;
Baada ya kutumia cocaine kwa muda mrefu punde unapoacha tu kutumia dalili zifuatazo hutokea;
UnyogovuUchovuKushindwa kuzingatia na kutokuwa makiniKukosa
uwezo wa kuwa na furaha au kusikia rahaKuongezeka kwa tama zaidi ya
kutumia cocaineKujisikia kuumwa, maumivu, baridi na kutetemeka.Ikitokea
mtu akitumia zaidi ya kiwango kinachotakiwa kwa muda mfupi yaani
overdose, kifo cha ghafla huweza kutokea kutokana na madhara yafuatayo;
Moyo kushindwa kufanya kazi.
Kiharusi,Degedege mara kwa mara na Mfumo wa hewa kushindwa kufanya kazi
Heroin
Hujulikana vilevile kama diamorphine, hutokana na mmea huitwao kitaalamu opium poppy. Heroin kwa mfumo wa Morphine hutumiwa hospitalini kama dawa ya maumivu makali ya ghafla (acute pain) kwenye maumivu makali ya kifua wakati wa shambulizi la moyo, na kwa maumivu ya mtu aliyepata ajali, vilevile baada ya upasuaji, na maumivu sugu kwenye kansa. Hivyo hutolewa kwa kuangalifu mkubwa.

Aina hii ya dawa
ya kulevya huweza kutumika kwa kuvuta kwa pua, kuvuta kama sigara na kwa
kuchoma kwenye mshipa. Siku hizi watu hutumia njia ya haja kubwa na
kwenye uke, ambapo kuta hufyonza heroin na kuanza kufanya kazi ndani ya
sekunde arobaini.
Heroin mara tu
baada ya kuingia kwenye damu kuenda kwenye mfumo wa neva na kukandamiza
ufanyaji kazi wake, ndio huweza kutumika kupunguza maumivu.
Dalili za mtu aliyetumia heroin
Dalili ambazo hutokea mara tu anapotumia Heroin:
Dalili ambazo hutokea mara tu anapotumia Heroin:
Kujisikia mwenye
furaha na rahaKupishana Kusikia hali usingizi na tahadhariMidomo kuwa
mikavuMisuli kuishiwa nguvuKuhema polepoleWarm skin flushingMikono na
miguu kuwa mizitokope za macho kulegea
Nini madhara ya matumizi ya muda mrefu ya heroin?
Madhara ya matumizi ya muda mrefu wa dawa hii ya kulevya hutokana zaidi na matumizi ya sindano na vifaa vingine visivyo salama
Madhara ya matumizi ya muda mrefu wa dawa hii ya kulevya hutokana zaidi na matumizi ya sindano na vifaa vingine visivyo salama
Maambukizi kwenye
kuta na milango ya moyoMaambukizi ya ini na virusi (kama hepatitis C na
HIV),Maambukizi ya figoMaambukizi ya mfumo wa hewaMaambukizi ya ngozi
na majipu
Dalili ambazo hutokea mara tu unapoacha kutumia heroin;
KutotuliaMaumivu ya misuli na mifupaKutapikaDalili hizi hufikia kilele ndani ya masaa 48 hadi 72 na hufika kikomo baada ya wiki.
Imetayarishwa na N.G.Shivji
najimshivji01@gmail.com
najimshivji01@gmail.com
Nicely said mr najim thanx for the lesson of all time appreciate it ..
ReplyDelete