Friday, 2 September 2016

UKWELI KUHUSU UGONJWA WA UTI :ATHARI KINGA NA MATIBABU YA UGONJWA WA UTI.

Asilimia kubwa ya Watanzania hawaujui vizuri ugonjwa wa UTI. Kumekwepo na maelezo kutoka kwa watu mbali mbali na wakati mwingine hata kwa wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa huu lakini bado watu wengi wanakanganyika na ukweli halisi.Leo nitajaribu kutoa maelezo walau kwa kina ili jamii iujue ugonjwa huu kinagaubaga.

Kwanza kabisa kirefu cha cha herufi UTI ni URINARY TRACT INFECTION ikimaanisha maambukizi kwenye njia ya mkojo.

Msomaji anapaswa kujua njia ya mkojo ni ipi, inaanzia wapi na inaishia wapi. Kwa ujumla njia ya mkojo inaanzia kwenye mrija wa mkojo kwa mwanaume na mwanamke. Mrija huu unajulikana kama URETHRA na ukishapata maambukizi ugonjwa sehemu hii unaitwa URETHRITIS.Njia ya mkojo inayofuata baada ya urethra ni BLADDER yaani kibofu.Wanawake wanakua na urethra fupi 4cm kulinganisha na wanaume 25cm hivo kupelekea kupata UTI kwa urahisi.



Kibofu kikipata maambukizi ugonjwa unajulikana kama CYCITITIS. Baada ya kibofu inafuata mirija miwili inayokwenda kwenye figo mbili. Mirija hii inaitwa URRETERS na ikishaambukizwa inajulikana kama URRETITIS.Na mwisho wa njia ya mkojo ni figo mbili yaani KIDNEYS na hizi figo zikishaambukizwa ugonjwa unajulikana kama NEPHRITIS.


Hivyo sababu huambatana na chanzo cha tatizo katika mojawapo ya sehemu husika, Mfano:
1. Ugonjwa wa sukari hufanya kiwango cha sukari kuwa kikubwa kwenye damu kwa vile mafigo kazi yake ni kuchuja damu hivyo ni kusema sukari huingia kwa wingi kiasi cha kusababisha vidudu bakteria kuzaliana kwa wingi kwenye mafigo au kibofu cha mkojo.

2. Madawa /sumu huchubua utando wa njia ya mkojo na kusababisha bacteria kuzaliana

3. Matatizo ya vijiwe kwenye figo/ mirija ya mkojo, kibofu, hufanya msongomano wa mkojo na Vijidudu huzaliana.

4. Maradhi ya Tunda Prostate gland huvimba na kufunga njia ya mkojo matokeo yake kuuzuia na kuuweka mkojo mda mrefu kwenye kibofu mpaka bacteria kuzaliana.
5. Tendo la ndoa, sexual intercouse unapata vijidudu moja kwa moja kutoka kwa mwanamke mwenye uambukizo

6. Kujichua, tendo hili mara nyingi watu hutumia mafuta au sabuni ambazo huwa zina kemikali zinazopenya kwenye mrija wa mkojo huwasha na kusababisha vidonda ambayo bacteria hukua na kazaliana

7. Usafi, aidha kwa kujikamua sana baada kukojoa, kutawaza maji machafu kutokuwa na hali ya unadhifu, huko chini kuna vijidudu ambavyo huishi baina ya njia ya haja kubwa na makorodani kutokana na hali ya ujoto humea vizuri na hupata nafasi ya kukuingia kwenye mirija kama utakuwa huna tabia ya kuwapunguza kwa usafi.


Sasa basi ni lazima tujue ni vimelea wa aina gani wanaoleta ugonjwa wa UTI.


Hapa nitajaribu kuonisha na kupanga vimelea katika makundi maalum.
Vimelea vinavyojulikana ni kama ifutavyo:
1. BACTERIA eg Streptococci, Staphylococci, E.Coli, H.Influenza, Proteus sp.Pseudomonas etc.
2. VIRUSES eg Clamydia tracomatis
3. FUNGI eg Candida albicans
4. TRICHOMONIASIS
5. SCHISTOSOMIASIS (kichocho)
6. PARASITES
7. GONORRHEA (kisonono).

Watoto wadogo mara nyingi wanapata UTI kutokana na kutobadilisha nepi kwa wakati na hivyo unyevu wa mikojo na mavi huvuta vimelea na kuleta maambukizi. Kwa watu wazima hasa wale wanaofanya ngono zembe wanapata magonjwa ya zinaaa kwa urahisi na hivyo wanakuwa tayari wana UTI. Kuna fikra kubwa imejengeka miongoni mwa jamii kuwa UTI inaletwa kwa urahisi kwenye vyoo vya kuchangia.


Image result for African baby in diapers
Dhana hii kwangu naweza kusema si sahihi hata kidogo kwa sababu wanaume wanakojoa kwa kuagiza mkojo kwa mbali kama risasi kwenye tundu la choo, sasa hao vimelea wanafuata mkondo wa mkojo kama unavyofanya umeme? Au wanaruka na kuja kuingia kwenye tundu la mkojo? Jibu ni hapana.Kwa wanawake wao wanajisaidia kwa kuchuchamaa, lakini hii sio sabau kua nyeti zao zinagusa kwenye sinki au shimo la choo na wala vimelea vya magonjwa vilivyomo chooni haviambukizi kamwe kwa ya mvuke.

Dalili za UTI zinaonekana kulingana na aina ya maambukizi.Lakini dalili kuu kwa watoto na watu wazima zinafanana nazo ni maumivu wakati wa kukojoa na pengine kutoka uchafu au usaha kwenye njia ya mkojo.Hizi ni dalili za UTI kulingana na aina ya maambukizi.Kama nilivotangulia kusema awali zipo aina tatu za UTI urethritis(maambukizi kwenye mrija wa mkojo),cystitis (maambukizi kwenye kibofu) na pyelonephritis(maambukizi kwenye figo)


 Urethritis dalili zake ni kupata maumivu wakati wa kukojoa
cystitis dalili zake ni kupata maumivu ya tumbo chini ya kitovu na saa nyingine kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu.
Pyelonephritis dalili zake ni Homa,kichwa kuuma,kichefuchefu,kutapika,maumivu ya tumbo sehemu za pembeni na mgongo kuuma.

MATIBABU:UTI ni ugonjwa unaotibika kabisa,pindi utapopata dalili hizi unashauriwa kufika hospital na kupata vipimo na matibabu sahihi.


JINSI YA KUJIKINGA NA UTI:
Eneo hili ni muhimu sana,watu wengi wamekua wakidhania kua UTI haiponi kutokana na sabau kua wamekua wakipata tena uti muda mfupi baada ya matibabu,ni kwa sabau watu hawazingatii jinsi gan ya kujikinga na ugonjwa huu.Hizi ni njia za kujikinga
Jisafishe kutokea mbele kwenda nyuma:Hii ndio sabau kubwa ya wanawake kupata UTI kwasababu wakati wa kujisafisha baada ya haja kubwa wanasafisha kwa kuvuta maji kutoka nyuma kwenda mbele ambapo wanabeba bacteria waliopo kwenye njia ya haja kubwa na kuwaleta kwenye njia ya haja ndogo hivo kupata maambukizi.



Vaa nguo za ndani zinazoweza kufyonza unyevunyevu sana sana nguo za cotton

Kunywa maji ya kutosha,Inashauriwa mtu kunywa angalau lita 2 na nusu kwa siku.
Pia unashauriwa kukojoa baada ya tendo la ndoa hii husaidia kutoa nje vijidudu vilivoingia kwenye mrija wa mkojo wakati wa tendo

0 comments:

Post a Comment